Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
TAARIFA KWA UMMA
Tume ya vyuo Vikuu (TCU) inautangazia Umma kuwa
baada ya kukamilisha mchakato wa maombi ya waombaji wa vyuo vikuu, vyuo Vikuu Vishiriki
na Taasisi za elimu ya juu kwa awamu ya kwanza, ya Pili na ya tatu, na matokeo
ya waombaji wote waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni kukamilika, Tume ya vyuo Vikuu
imebaini kuwa bado kuna waombaji takribani 5,301 ambao bado wako kwenye mfumo
na hawajakamilisha maombi yao.
Tume imebaini pia kuwepo kwa idadi kubwa ya
waombaji hasa wenye Stashahada ambao hawakuomba kabisa kutokana na matokeo yao ya mitihani
kuchelewa kufika Baraza za Vyuo Ufundi (NACTE)
- Awamu hii itawahusu:
- Waombaji ambao bado wako ndani ya mfumo ambao hawajapata nafasi
- Waombaji wapya ambao hawakuwahi kuomba awali; na
- Waombaji walio na sifa linganifu ambao hawakukamilisha taratibu za uombaji hapo awali
Kutokana na sababu tajwa hapo juu, tume
inautangazia Umma kuwa itafungua Mfumo (CAS) kwa siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi Jumatano tarehe 26 Oktoba 2016
ili kuruhusu Makundi tajwa hapo juu
kuingia kwenye mfumo kutuma maombi.
Waombaji wa awamu ya Nne wanasisitizwa
kuzingatia yafuatayo:
- Kuhakikisha wanaomba kozi walizo na sifa stahiki
- Kuhakikisha wanakamilisha maombi yao kiufasaha
- kuhakikisha wanajiridhisha na nafasi zilizopo kwa kuzingatia viwango vyao vya ufaulu.
Aidha Tume inapenda kuujulisha Umma
kwamba kozi zote zisizo onekana kwenye mfumo kwa sasa kuwa zimejaa.
Baada ya tarehe tajwa hapo juu tume
itafunga rasmi zoezi la udahili kwa mwaka2016/17 ili kuruhusu michakato mingine
ya Bodi ya Mikopo na Vyuo kuendelea.
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
21/10/206
0 comments:
Post a Comment