TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA TCU
TANGAZO KWA UMMA
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma
kuwa imekamilisha kuchakata maombi ya kujiunga
na Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu kwa awamu ya kwanza na ya pili. Orodha na majina
ya walichaguliwa yameshapelekwa vyuoni kwa ajili ya kuiidhinishwa na Seneti za vyuo
husika. Baadhi ya vyuo vimeshaanza kuyatangaza.
Hata hivyo, kuna waombaji ambao bado wako kwenye
mfumo na hawajachaguliwa kwenye kozi yoyote
kati ya walizoomba kutokana na sababu mbalimbali
kama ifuatavyo
• Ushindani mkubwa katika programu
za masomo walizoomba ukilinganisha na ufaulu wao
•Waombaji kushindwa kukamilisha taratibu za uombaji; na
•Waombaji kutokuwa na sifa kwa kozi walizoziomba.
Kutokana na hali hiyo, Tume inautangazia umma kuwa
mfumo wa udahili utafunguliwa tena kwa
awamu ya tatu mnano tarehe 10 mpaka tarehe 16 Oktoba 2016 ili kuruhusu waombaji
na aina hii kufanya uchaguzi
upya au kukamilisha maombi yao.
Tume inapenda kufafanua kuwa programu za masomo zisizoonekana kwenye mtandao zimekwishajaa,
hivyo waombaji watalazimika kuomba zile tu zinazoonekana mtandaoni.
Zoezi hili la uombaji kwa awamu ya tatu linawahusu waombaji wenye sifa za
kidato cha Sita, Stashahada na sifa
linganishi. Hakutakuwa na malipo yoyote kwa waombaji hawa. Tume inapenda kusisitiza
kwamba awamu hii haitawahusu waombaji wapya, ambao hawakuwahi kujisajili wala
kuomba udahili kwa awamu ya kwanza na ya pili.
Imetolewa
na
Katibu
Mtendaji
Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania
10/10/2016
Source:
http://www.tcu.go.tz/images/documents/CALL_FOR_THIRD_ROUND_OF_APPLICATIONS-2016-17.pdf
0 comments:
Post a Comment