KUONGEZWA KWA MUDA WA USAJILI NA KUCHAGUA MASOMO SARIS

on Monday, December 5, 2016
TANGAZO MUHIMU
KUONGEZWA KWA MUDA WA USAJILI NA KUCHAGUA  MASOMO SARIS
HADI TAREHE 8 /12/2016 WANAFUNZI WA  DIPLOMA NA CHETI
Napenda kuchukua fursa hii kuwataarifu wanafunzi wote ombi letu la kuomba kwa menejment juu ya mda kuongezwa hususani kwa diploma na certificate , Mda wa usajili  umeongezwa kwa ajili ya usajili ili wanafunzi waweze kufanya usajili huo na aweze kufanya  mitihani na  ni lazima alipe ada yote ya semester ya kwanza pamoja na Bima ya Afya
  •  Kwa yeyote ambaye hana namba ya invoice basi aende kwa watu wa accounts akapewe invoce namba na aweze kulipia Bima yake maana ni lazima
  •  Kwa Mwanafunzi mwenye Bima Kutoka makampuni mengine basin aye awasilishe uhalali wa bima zao kwamba zipo active kwa kupeleka nakala ya copy ya bima yako yenye uthibitisho kutoka kwa kampuni ya bima husika.
  •  Ili uweze kufanya mtihani na kuona course work lazima uwe umesajiliwa na umesajili  masomo yako yote ya semester ya kwanza( Module Registration ) bila ya kusahau kufanya Course Evaluation katika kila somo ambalo litakua uploaded na Mwalimu Husika.
  •  Kwa Wanafunzi ambao wanarudia masomo au kuyabeba (Carryforwad and Repeat Module ) wanapaswa pia kusajili masomo yao wanayo yarudia kwa semester hii ya kwanza na  wa repeat Module lazima  ulipie somo lako kwa kutumia invoice number na usajili katika akaunt yako ya saris pamoja na bima
  • Kama ulisahau kusajili masomo yako au kupick wakati wako ni sasa inabidi ufanye taratibu hizo.
  • Hakikisha Unatatua matatizo yako yote ambayo yanahusiana na saris usije ukasema ukujua maana hakitakuwa na muda wa ziada tena.


ANGALIZO
Hakutakuwa na Muda mwingine utakao ongezwa wa ziada kama hutokamilisha hayo basi itakupaswa ufanye taratibu zingine za kuhairisha mwaka wa masomo hadi mwakani tena

Tafadhali Ndugu wanafunzi nawaomba muweze kuzingatia mambo Muhimu  Ikiwa ni Pamoja na
  
   Ø  Kupita kwenye mbao za Matangazo kila mara na kutembelea kwenye blogu ya wizara ya elimu (cbeeducation.blogspot.com)
   Ø  Kuzingatia Sheria na kanuni za Mitihani
   Ø  Pia tuwasilkilize Viongozi wetu wa Madarasa na Viongozi Wengine punde watuleteapo  taarifa Zenye umuhimu ambazo wanatupatia madarasani na kuzitekeleza Mapema kabla ya hazijatuathiri
Tafadhali taarifa hii ya Muhimu Mjulishe na mwenzako kwa haraka sana  

KUPITA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NI MUHIMU SANA
Claud A Ndikwege

Waziri wa Elimu na Masomo ya Jioni
Nakala:
            Quality Assurance
            Dean of Students
            President Office 



0 comments:

Post a Comment