JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA
MTWARA
(Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)
Kumb. Na. AC.253/525/01/147 31 Mei,2025
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Halmashauri ya Wilaya
ya Mtwara imepata
idhini ya utekelezaji wa Kibali cha Ajira Mpya chenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha Tarehe 29 Aprili, 2025 kwa ajili ya kuajiri Mwandishi Mwendesha
Ofisi II nafasi 2 na Dereva II nafasi 2 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtwara anawatangazia watanzania wenye sifa na nia ya kufanya
kazi katika Halmashauri hiyo, kuomba nafasi za kazi zifuatazo:
1.0
MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA
LA II - NAFASI 2
1.1
KAZI/ MAJUKUMU
YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri
ii. Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
iii.
Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine
iv.
Kutafuta majalada na nyaraka
zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
v.
Kupokea majalada na kusambaza
kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika
vi. Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika
vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali
viii.
Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form
Six) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe amefaulu somo la Hatimkato ya
Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za
kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka
chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.3
MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni TGS C1.
2.0
DEREVA DARAJA LA II - NAFASI
2
2.1
KAZI/ MAJUKUMU
YA DEREVA
i.
Kukagua gari kabla
na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama
wa gari;
ii.
Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye
safari za kikazi;
iii.
Kufanya matengenezo madogo
madogo ya gari;
iv.
Kukusanya na kusambaza
nyaraka mbalimbali;
v.
Kujaza na kutunza
taarifa za safari
zote katika daftari
la safari;
vi.
Kufanya usafi wa gari; na
vii.
Kufanya kazi nyingine
kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
viii.
Pamoja na kazi zingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.
2.2
SIFA ZA MWOMBAJI
2.3
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato
cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo
wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali
pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika. Wawe
wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving Course)
yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.4
MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni TGS B1
MASHARTI YA JUMLA
i.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia
miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini
Serikalini;
ii.
Waombaji wenye ulemavu
wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea
ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika
Utumishi waUmma
iii.
Waombaji wote waambatishe maelezo
binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika,
namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na
majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iv.
Waombaji waambatishe maelezo
binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anuani na namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika;
v.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya
Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya
Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificates,
- Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, - Computer Certificate, - Vyeti vya
Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards);
vi.
“Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii.
Waombaji waliosoma nje ya Nchi
wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA
na NACTE).
viii.
Waombaji waliostaafishwa katika
Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa
Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.
Waombaji kazi ambao tayari ni
waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe
na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,
2010.
x.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.
Waombaji kazi wa kada ya Dereva II
wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva
vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika
xii.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 17 Juni, 2025
xiii.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua
yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua
hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi
Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya Mtwara,
S.L.P. 528,
MTWARA.
xiv.
Maombi yote yatumwe
kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani
ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti
ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment
Portal').
xv.
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu
ulioainishwa katika tangazo
hili
HAYATAFIKIRIWA.
Imetolewa na:
Abeid A. Kafunda
MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI
YA WILAYA MTWARA
Source :https://www.ajira.go.tz/
0 comments:
Post a Comment