TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA TANDAHIMBA
(Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)
Kumb. Na. JB.124/294/01B/98 05 Juni, 2025
TANGAZO LA NAFASI
ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba amepata
Kibali cha Ajira Mpya chenye kumb. Na. FA.
97/288/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 chenye nafasi ya Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (2) na Dereva
Daraja la II (8) kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Tandahimba
anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye
sifa na nia ya kufanya
kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kuomba maombi ya nafasi za kazi zifuatazo:
,
1.0
MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA
LA II - NAFASI 2
1.1
KAZI/ MAJUKUMU
YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI
i.
Kuchapa barua, taarifa
na nyaraka za kawadia na za siri
ii.
Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
iii.
Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine
iv.
Kutafuta majalada na nyaraka
zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
v.
Kupokea majalada na kusambaza
kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika
vi.
Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada
na nyaraka sehemu
zinazohusika
vii.
Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mablimbali
viii.
Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
1.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.3
MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni TGS C1.
2.0
DEREVA DARAJA LA II - NAFASI
8
2.1
KAZI/ MAJUKUMU
YA DEREVA
i.
Kukagua gari kabla
na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama
wa gari;
ii.
Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye
safari za kikazi;
iii.
Kufanya matengenezo madogo
madogo ya gari;
iv.
Kukusanya na kusambaza
nyaraka mbalimbali;
v.
Kujaza na kutunza
taarifa za safari
zote katika daftari
la safari;
vi.
Kufanya usafi wa gari; na
vii.
Kufanya kazi nyingine
kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
viii. Pamoja na kazi zingine utakazopangiwa na Mwajiri wako.
2.2
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja
E au C ya uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka
mmoja (1) bila kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia
sifa ya kupata madaraja husika. Wawe wamehudhuria mafunzo
ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic
Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
2.3
MSHAHARA
Ngazi ya Mshahara ni TGS B1.
MSHAHARA YA JUMLA
i.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia
miaka18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini
Serikalini;
ii.
Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao
kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi waUmma
iii.
Waombaji
wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae)
yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe
(E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iv.
Waombaji waambatishe maelezo
binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za
kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
v.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya
Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya
Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Postgraduate/Degree/Advanced
Diploma/Diploma/Certificates, - Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI,
- Computer
Certificate, - Vyeti
vya Kitaaluma (Professional Certificate from
Respective Boards);
vi.
“Testmonial“,
‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii.
Waombaji
waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na
Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
viii.
Waombaji waliostaafishwa katika
Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa
Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.
Waombaji
kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba,
2010.
x.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za
kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.
Waombaji kazi wa kada ya Dereva II
wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva
vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
xii.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 18/6/2025
xiii.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya
maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo
ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba,
S.L.P 03,
TANDAHIMBA -
MTWARA.
xiv.
Maombi yote yatumwe
kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani
ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti
ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment
Portal').
xv. Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA TANDAHIMBA
Source :https://www.ajira.go.tz/